Rais wa Marekani

Rais wa Marekani ni mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali ya Marekani. Rais ni afisa anayechaguliwa na wawakilishi wanaopatikana katika uchaguzi wa urais unaotekelezwa katika kila jimbo la nchi. Kati ya mamlaka na majukumu mengine, ibara ya II ya Katiba ya Marekani inampa rais jukumu la kutumikia kiaminifu sheria za nchi, humfanya rais kuwa mkuu wa majeshi. Akiwa mkuu wa serikali anawateua mawaziri na washauri wake. Anapendekeza majina ya majaji, na mapendekezo yake yanahitaji kibali cha senati (bunge la juu). Rais ana haki ya kusamehe wakosaji waliohukumiwa chini ya sheria ya maungano ya Marekani. Kutokana na Marekani kuwa sasa kama nchi babe, rais wa Marekani huonekana kama mtu mwenye nguvu zaidi katika dunia. Rais huchaguliwa kwa muda wa miaka minne. Tangia mwaka 1951, utawala wa marais umekuwa ni mihula miwili kutokana na marekebisho ya katiba ya 22. Tangu kuanzishwa kwa Marekani walikuwepo marais 44 waliochaguliwa na kuhudumia jumla ya mihula 56 ya muda wa miaka isiyozidi minne Tarehe 20 Januari 2017, Donald Trump amekuwa rais wa arobaini na tano.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search